29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

OLE NASHA: WABUNGE, WAHADHIRI ACHENI UKWARE WAACHENI WANAFUNZI WASOME

Gabriel Mushi, Dodoma

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ametoa wito kwa wabunge kutojihusisha na vitendo vya kingono na wafunzi wa vyuo vikuu na wawaache wasome.

Pia ametoa rai kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapopata taarifa za walimu na wahadhiri wa vyuo vikuu kuwafelisha wanafunzi kwa kutaka rushwa ya ngono.

Kauli hiyo ya OleNasha imekuja baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) kusema kuwa baadhi ya wahadhiri wanajifanya ni vidume vya mbegu katika kuwafelisha wanafunzi hao.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema serikali imelipokea suala hilo na haina uvumilivu kwa vitendo hivyo.

“Pia mwanafunzi hadi ahesabike kuwa amefeli haitokani na mtazamo wa mwalimu mmoja tu, kuna taratibu zimeweka kupitia ‘marks’ (alama) ambazo amepata kutokana na kazi zake ili kuamua amefaulu au amefeli. Hata kama ilitokea mwalimu mmoja amefanya vitendo hivi, hii haiwezi ikaathiri ufaulu kwa vitendo hivi.

“Vyuo vikuu ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), vina taratibu maalumu ya kushughulikia masuala haya ya unyanyasaji wa kijinsia lakini wanafunzi wengi hawatumii msaada huu. Tunawasihi kama watapata matatizo kama haya waende kwa mshauri wa wanafunzi (dean of student),” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles