BERLIN, UJERUMANI
WAZIRI wa Maendeleo wa Ujerumani, Gerd Muller, amesema nchi yake na Irak zitashirikiana kutekeleza zoezi la kuwarudisha nyumbani wakimbizi 10,000 wa Irak.
Muller amesema Ujerumani na Iraq zimekubaliana kushirikiana kwa undani zaidi ili kuwasaidia kurudi nyumbani Wairaki hao waliokuwa wameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Ujerumani.
Muller aliyekuwa ziara Irak, pia amesema Ujerumani na Irak zitafanya kazi kwa pamoja ili kuwapa fursa za elimu na ajira Wairaki wanaorejea kwao.
Kati ya Wairaki 240,000 wanaoishi nchini Ujerumani kwa sasa, 12,000 miongoni mwao hawajafanikiwa kupata hifadhi ya ukimbizi.