25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Nchimbi: Hatutakuwa na huruma na wagombea wa CCM

Na Mohammed Ulongo, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa rai kwa wagombea wa CCM kuwa chama hakitakuwa na huruma dhidi ya mgombea yeyote ambaye atashinda Uchaguzi na kushindwa kuwatumikia wananchi, kuwaumiza pamoja na kutotatua changamoto za wananchi katika maeneo yao.

 Hayo ameyabainisha mapema hii leo Novemba 26,2024 katika mkutano wake wa hadhara wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika eneo la Mbagala Kingugi  jijini Dar es salaam.

“Ninajua kwa uzito wa Kampeni tulizofanya kuwanadi wagombea wetu kama CCM, sina Shaka kwamba wote hapa mtashinda kwenye mitaa yenu,  rai yangu muende mkafanye kazi ya kuwasaidia Wananchi kutatua kero zao na sio kwenda kuwaumiza” amesema Dkt Nchimbi.

Aidha Dkt Nchimbi amewahakikishia wana CCM kuwa kesho hadi kufikia Saa 4 asubuhi  Chama hicho kitakuwa kimeugalagaza upinzani kwa Tofauti ya kura nyingi kwenye Mitaa mbalimbali.

Hata hivyo Katibu Nchimbi amesema kuwa kuwepo kwa uchaguzi huu wa serikali za mitaa chama Cha Mapinduzi kimefanikiwa kufanya kampeni katika vijiji na vitongoji vyote nchini katika kuhakikisha wanajizolea ushindi mnono wa matokeo ya jumla ya Uchaguzi wa serikali za mitaa.

Pamoja na kampeni zilizofanywa katika maeneo mbalimbali nchini katibu Nchimbi amehitimisha kwa kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuamua chama kitakacho beda matatizo ya watanzania na kuyatatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles