24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

MWANA MFALME UINGEREZA APATA MTOTO WA KIUME

LONDON, UINGEREZA


MKE wa mwanamfalme wa Uingereza, Prince William, Kate amejifungua mtoto wa tatu wa kiume katika hospitali ya Mtakatifu Mary mjini hapa jana.

Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo, hali ya afya ya mama na mtoto, ambaye alizaliwa saa saba mchana za Afrika Mashariki, inaendelea vizuri.

Ukoo mzima wa kifalme umepata taarifa ya ujio wa mtoto huyo na wana furaha kwa habari hizi njema, huku wafuasi wakiwa wamejazana nje ya hospitali, wengine wakinywa na kucheza.

Hadi sasa jina la mtoto mpya bado halijatangazwa, huku taarifa kutoka makazi ya malkia zikisema William alikuwepo wakati mtoto huyo akizaliwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, majina ambayo William anayapenda ni Arthur, Albert, Frederick, James na Philip.

Salamu za pongezi zimetumwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Theresia May na anawatakiwa furaha na maisha mema yajayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles