32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

MGEJA: KUJIUZULU MAWAZIRI NI BURE

Na PASCHAL MALULU


MWENYEKITI wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo, Khamis Mgeja, alisema ingawa serikali inapambana na wabadhirifu na wezi wa rasilimali za umma,   kitendo cha mawaziri kujiuzuru  bila kuwajibishwa hakiwanufaishi wananchi ambao wako katika umaskini mkubwa.

Mgeja alitoa kauli hiyo mjini Kahama juzi alipokutana na wazee wa   Kisukuma nyumbani kwake mtaa wa Nyasubi.

Alisema ingawa kila tatizo la wizi na upotevu wa mali za umma linapotokea imekuwa kasumba ya mawaziri kujiuzuru jambo hilo halimnufaishi Mtanzania kwa sababu hakuna kitu chochote kinachobadilika hasa maisha yao na huduma za  jamii.

“Wakati umefika Watanzania tuambizane ukweli kinachosababisha mianya ya wizi na ubadhirifu wa rasilimali za nchi ni mfumo uliojengwa ukatungiwa sheria  na kusimamiwa na watawala wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wa awamu zote,” alisema Mgeja.

Mgeja ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 alipojiuzuru, alisema kitendo cha mawaziri kujiuzuru mara kwa mara ni sawa na kuwatoa kafara.

Wazee hao walishauri kwa hali ya nchi ilivyo kwa sasa hakuna haja kutafuta mchawi au kuendelea kufukua makaburi kwa sababu hakuna atakayebaki salama lakini kuna haja ya kuurekebisha mfumo ulioifikisha nchi hapo ilipo.

Kiongozi wa wazee hao, Jozia Ngwanateleza, kwa niaba ya wenzake alimuomba Rais Dk. John Magufuli kukamilisha mchakato wa katiba mpya.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Na bado inaendelea kwa awamu hii. CCM ndicho chama kikuu kilichowaibia Watanzania. Mfumo mzima wa CCM ni mbovu. Watu wengi wanalindana. Sababu ya uwingi wao, na huenda asilimia kubwa yao wamehusika kwa mambo haya. Hakuna hata mmoja mwanaCCM wa ngazi za juu yupo tayari kuwaadhibu hawa. Na bado watu wanakiunga mkono. Kila anayepata madaraka, wengi wametoa hongo, na wengi wao ndo mafisadi wakuu. Huwezi kuinyoosha nhi kwa kuwaachia tu waondoke. Wafilisiwe kila kitu, wafungwe miaka mingi tu. Au la bila hii katiba kuwekwa sawa. Bado viongozi wa CCM wanaendelea kuhujumu na kutokufuata sheria. Hata kupeana vyeo, mikataba bado ukiwa nje ya CCM hupati. ndo maana wengi wanakimbilia huko wapewe vyeo na wazidi kujinufaisha. Ni mchezo mchafu, na kuwachezea Watanzania kama vitoto visivyo na akili. Ebu wengi muuunge mkono na mumuunge mkono ndugu Khamisi mgeja ili nchi hii iwe na nsimamo thabiti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles