30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

MERKEL AANZA JUHUDI ZA KUUNDA SERIKALI MPYA UJERUMANI

BERLIN, UJERUMANI

VIONGOZI  wa chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union (CDU) cha Kansela Angel Merkel kimekutana jana asubuhi kutathimini matokeo ya uchaguzi mkuu na kuzungumzia uundaji wa serikali mpya ya ushirika.

Chama hicho kimejipatia asilimia 33 tu ya kura, kiwango cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1949; kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa jana asubuhi.

Ushindi huu wa nne mfululizo wa Kansela Merkel aliyeko madarakani tangu mwaka 2005, ni mchungu kwake.

Na dalili za mwanzo za malalamiko zimechomoza upande wa washirika wao wa kihafidhina wa Bavaria, Christian Social Union (CSU) wanaomhimiza Kansela Merkel aelemee zaidi kulia.

Msimamo huo unatokana na ukweli kwamba sehemu ya wapigakura wa kihafidhina wa chama chake wamekipigia kura kile cha siasa kali za mrengo wa kulia, Chaguo Mbadala kwa Ujerumani (AfD), ambacho kinapinga wahamiaji na Waislamu.

Baada ya miaka 12 madarakani, si rahisi kuibuka kuwa chama chenye nguvu zaidi. Lakini sasa changa moto kubwa iko mbele yetu. AfD wanawakilishwa bungeni. Tunataka kuwatanabaisha na kurejesha imani ya wale waliowapigia kura kwa kuzingatia kwa makini zaidi madai yao na kwa kuiendesha nchi vyema zaidi.”

AfD wamepatia asilimia 12.6 ya kura kwa kufanya kampeni wakimuiga Rais wa Marekani Donald Trump na kushadidia msimamo wa Uingereza wa kujitoa Umoja wa Ulaya (EU).

Hata hivyo, ufa umejitokeza miongoni mwa viongozi wa AfD kuhusu msimamo unaobidi kufuatwa na chama hicho.

Markel kwa sasa anatafuta chama cha kuungana nacho kuunda serikali, ambapo mazungumzo ya hatua hiyo yanaweza kudumu miezi kadhaa na pindi yakishindwa kuleta tija, uchaguzi mpya utaitishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles