24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

UCHUKUZI SHEHENA KWA NDEGE KIMATAIFA WAPOROMOKA

Idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini imeendelea kupanda mwaka 2017 huku uchukuzi wa shehena kwa usafiri huo ukishuka.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amesema hayo leo Jumatatu Septemba 18, jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia kongamano la siku mbili litakaloanza kesho kujadili changamoto kubwa tisa zinazoikabili sekta hiyo ikiwamo kuporomoka kwa uchukuzi wa shehena ambazo nyingi zinatoka nchini lakini zinasafirishwa na nchi jirani.

“Tuna kitengo chetu cha idara ya takwimu kinaonyesha dhahiri uchukuzi wa shehena hapa nchini unashuka na wa abiria unapanda, hivyo kikao cha kesho ndio kitakachotoa majibu kwanini tunashuka.

“Inasikitisha kuona shehena za minofu ya samaki mkoani Mwanza inasafirishwa kwa mtumbwi na kupelekwa kiwanja cha Entebbe nchini Uganda na si Uwanja wa Ndege wa Mwanza, pia maua yanayolimwa mkoani Arusha yamekuwa yakisafirishwa kwenda kiwanja cha Ndege cha Jomo Kenyatta na kukiacha kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KIA),” amesema Johari.

Pamoja na mambo mengine, Johari amesema kongamano hilo ndilo litakaloleta mafanikio ya kufikia uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2020.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles