Na TIGANYA VINCENT
–Â SIKONGE
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge, imesema itaanzisha kilimo cha korosho kama zao mbadala la biashara litakaloungana na lile la tumbaku ikiwa ni hatua ya kuandaa malighafi kwa ajili ya viwanda.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Sikonge na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Simon Ngatunga, wakati akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Alisema hivi sasa wameshaandika barua kwa Bodi ya Korosho nchini kwa ajili ya kupatiwa miche ya mikorosho ili kupanda maeneo mbalimbali wilayani humo.
Ngatunga aliongeza kuwa udongo wa Sikonge unafaa kwa ajili ya zao la korosho jambo ambalo linatoa fursa kwa wakazi hao kuwa zao jingine linaloweza kuwapatia fedha.
Alisisitiza kuwa zao hilo pia litasaidia kupunguza uharibifu wa misitu kwa wakulima kutotegemea tumbaku pekee kama zao la biashara.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, aliwaagiza viongozi wote katika halmashauri zote nane mkoani humo kuhakikisha wanasisitiza kilimo cha korosho, alizeti na pamba kwa wilaya ya Urambo, Igunga, Kaliua, Nzega na Uyui.
Alisema zoezi hilo linalenga kuwa na malighafi za kutosha kwa ajili ya Kiwanda cha Nyuzi Tabora na kuweza kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti.
Mwanri alisisitiza kuwa ardhi ya Tabora inakubali mazao mbalimbali na hivyo wanataka kutumia fursa hiyo ya uzuri wa ardhi kumwongezea mkulima wigo wa mapato na kwa upande mwingine kuziongezea halmashauri mapato ya ndani.
Mkuu huyo wa mkoa pia aliwaagiza maofisa ugani wote mkoani hapa kuwahamasisha wakulima kuanza maandalizi ya kilimo cha msimu ujao ili waweze kutumia mvua za mwanzo vizuri.
Alisema mvua za mwanzo ndizo zitakazowawezesha kuvuna mazao mengi