Seoul, Korea Kusini
RAIS wa Korea Kusini aliyetimuliwa madarakani, Park Geun-hye, ameondoka rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo mjini Seuol.
Park ameondoka Ikulu na kwenda nyumbani kwake Kusini mwa Seoul, kwa mujibu wa msemaji wake Ikulu, Kim Dong-jo.
Alifukuzwa baada ya Mahakama ya Katiba nchini humo kuafiki uamuzi wa kuondolewa kwake kwa kashfa ya kupotea kwa mabilioni ya fedha wakati wa utawala wake.
Park sasa amepoteza uwezo wa kutofunguliwa mashtaka ambao marais huwa nao, na huenda akakabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa fedha.
Serikali ya Korea ya Kaskazini imepongeza kuondolewa kwake akiwa ni mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo.