31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAHISA MWINGINE JAMII FORUMS MBARONI

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam


 

Mike Mushi
Mike Mushi

MMOJA wa wanahisa wa Jamii Media inayoendesha mitandao ya JamiiForums na Fikra Pevu, Mike Mushi, amehojiwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kati, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Mushi anatuhumiwa kutumia mtandao bila kusajili kikoa cha dot Tz kama sheria inavyotaka.

Hata hivyo, baada ya mahojiano hayo Mushi alidhaminiwa na kuondoka kituoni hapa.

Wakati hayo yakiendea, upande wa Jamhuri umedai kwa mara nyingine kwamba upelelezi wa kesi ya kuwa na anuani za tovuti ambazo hazijasajiliwa Tanzania inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo haujakamilika.

Taarifa za kutokamilika kwa upelelezi huo zilitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa.

Jamhuri waliomba kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 16, mwaka huu kwa kutajwa tena.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa Melo anadaiwa kutenda makosa yanayomkabili kati ya Desemba 9 mwaka 2011 na Desemba 13 mwaka jana katika maeneo ya Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Inadaiwa akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii  Media Co Ltd unaofanya kazi chini ya sura ya 212 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, wenye hati ya usajili namba 66333, aliutumia mtandao wa Jamii Forums.com ambao haujasajiliwa katika anuani za tovuti za Tanzania.

Inadaiwa kati ya Januari 26 mwaka jana katika maeneo ya Mikocheni, Kinondoni akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo wa Jamii  Media Co Ltd  ambao unaendesha tovuti ya kijamii ya JF,  wakati akijua Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kuhusu mawasiliano ya kimtandao ambayo yalichapishwa katika tovuti yake kwa njia ya kuzuia uchunguzi huo, alishindwa kutekeleza amri ya kutoa data alizonazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles