24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

DC SHINYANGA AKAGUA GHALA LA TAIFA

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro

Na KADAMA MALUNDE-SHINYANGA

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga mkoani hapa, Josephine Matiro, ametembelea ghala la kuhifadhia chakula Kanda ya Shinyanga,  huku akiwataka wananchi kupuuza taarifa za uhaba wa chakula nchini.

Mkuu huyo wa wilaya alitembelea ghala hilo jana huku akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kwa lengo la kujionea hali halisi ya akiba ya chakula na kusema kipo cha kutosha.

“Itakapofikia hatua kuwa kuna ulazima wa chakula cha msaada kwa kaya ambazo hazina kabisa zimezidiwa kwa kukosa chakula, ifahamike kuwa tunacho chakula cha kutosha kimehifadhiwa vizuri kwenye ghala letu hili,” alisema Matiro.

Akizungumzia hali ya chakula katika ghala hilo, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Shinyanga, Mary Shangali, alisema hadi sasa kanda hiyo inayounda mikoa minane ina jumla ya tani 9,146.916 na wanatarajia kupokea chakula tani 10,000 kutoka Mpanda mkoani Katavi.

“Katika Kanda ya Shinyanga yapo maghala manne yaliyohifadhi chakula ambapo ghala la Bukene lililopo mkoani Tabora kuna tani 2,898.994, ghala la Shinyanga tani 6,050.969, ghala la Kasulu lililopo mkoani Kigoma  tani 196.629 hivyo kuna jumla ya tani 9,146.916,” alisema Shangali.

Alisema Juni mwaka jana Jeshi la Magereza walikuwa na tani 4,035 na walichukua tani 1,105 hivyo kubakiwa na tani 2,000 ambazo bado hawajachukua hadi sasa katika mgawo wao.

Shangali alisema kanda hiyo inajumuisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Tabora, Kigoma, Geita, Kagera na Shinyanga.

Kwa upande wake Ofisa Ugavi kutoka Hifadhi ya Kanda ya Shinyanga, Bitteme Mgabo alisema wamekuwa wakitoa chakula kwa maombi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles