Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital
Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, imejitokeza kusaidia waathirika wa kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo kwa kutoa fedha kiasi cha Sh milioni 20 ili kusaidia juhudi za uokoaji zinazoendelea.
Halotel ikiwa moja ya Kampuni ya Mawasiliano hapa nchini inayotoa huduma za mawasiliano kama kupiga simu, kutuma sms, huduma za Intanet pamoja na huduma za kifedha za halopesa, imeona ni vema kushika mkono waathirika wa Kariakoo na jamii nzima kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam eneo la Kariakoo, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Halotel, Roxana Kadio, wakati wa kukabidhi kiasi cha fedha cha milioni 20, amesema kuwa Halotel imeguswa na sana na janga hilo hivyo imeona ni budi kushirikiana na serikali katika juhudi za uokozi.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga, amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha kampuni ya Halotel kujitokeza kusaidia katika janga liliotokea Kariakoo, hivyo amewasihi watanzania wengine wajitokeze na waige kampuni hiyo.
Hata hivyo katika kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Halotel inahakikisha kuwa kati ya msaada unaotolewa katika kutatua na kuokoa watu kwenye janga hili ambapo kampuni hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na jamii katika kipindi hiki kigum