Juliana Samwely TUDARCo
Mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Emmanuel Cherehani, amewahimiza wananchi wa jimbo hilo umuhimu wa kuendelea kupata chanjo ya Uviko-19.
Cherehani ametoa rai wakati akinadi sera zake jimboni Ushetu, Wilayani Kahama katika kampeni zinazoendelea za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo baada ya aliyekuwa mbunge wake Elias Kwandika kufariki Agosti mwaka huu.
Pia kupitia kampeni hizo alitoa elimu ya sensa inayotarajia kufanyika mwakani kwa kuwakumbusha wananchi kutambua umuhimu wa suala hilo.
Aidha amesema endapo atachaguliwa atakamilisha ahadi zilizoahidiwa na mtangulizi wake marehemu Kwandika.
“Nitatimiza ahadi zote zilizoahidiwa, nitaleta maji yatawafikia hadi nyumbani kwani nishazungumza na Rais Samia Suluhu Hassan na amekubali, nitaleta umeme na kutakuwa na uhuru wa kufanya biashara katika wilaya hii,”amesema Cherehani.