27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wahudumu wa afya Mbika wamchefua Katibu UVCCM

Neema Paul, TUDARCO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Tanzania(UVCCM), Kenan Kihongosi  ameagiza  kuchukuliwa hatua za kiutendaji wahudumu wa  kituo cha afya  cha Kijiji cha  Mbika, kilichopo jimbo la Ushetu Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga baada ya kuwepo kwa  malalamiko kutoka kwa wananchi juu  ya utoaji  huduma usioridhisha.

Kihongosi amezungumza hayo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo baada ya kufariki kwa aliyekua mbunge wake Elias Kwandikwa  ambapo ametaka kupata maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa halmashauri kwa nini dawa hazipatikani katika kituo hicho  hadi  wakanunue maduka ya nje yanayomilikiwa na wahudumu  hao.

Amesema pia wahudumu wa kituo  hicho  cha afya  wanatoa lugha chafu kwa wagonjwa  wanapokwenda  kupata matibabu.

“Wagonjwa wakija hapa mnawatukana ,mnawafokea mnasahau kuwa wao ndio serikali na sisi tupo hapa  kwa ajili ya kuwahudumia wao hii si haki,” amesema.

Aidha Kihongosi ametoa onyo kwa tabia ya baadhi ya wauguzi kuacha  tabia ya kuchukua dawa hospitalini hapo na kuzipeleka kwenye maduka yao binasfi kwani kufanya hivyo ni kuwaumiza wananchi wenyewe na kutoa maagizo kwa Emmanuel Cherehani ambaye ni mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kufumbia macho suala hilo na kuwawajibisha wale wote wanaohusika

“Unaenda hospital unaambiwa dawa hakuna lakini nenda duka fulani utapata hiyo dawa sasa hii si sawa? amehoji katibu huyo.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM-Vijana, Mussa Mwakitinya ametoa rai kwa wananchi wa Mbika kuchagua kiongozi bora ambaye anaweza kusimama na kuwawakilisha  bungeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles