29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mgombea ubunge Ushetu ahimiza wananchi kupata chanjo

Juliana Samwely TUDARCo

Mgombea  ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Emmanuel Cherehani, amewahimiza wananchi wa jimbo hilo  umuhimu wa kuendelea kupata chanjo ya Uviko-19.

Cherehani ametoa rai wakati akinadi sera zake jimboni Ushetu, Wilayani Kahama katika kampeni zinazoendelea za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo baada ya aliyekuwa mbunge wake Elias  Kwandika kufariki Agosti mwaka huu.

Pia kupitia kampeni hizo  alitoa elimu ya sensa inayotarajia kufanyika mwakani kwa kuwakumbusha wananchi kutambua umuhimu wa suala hilo.

Aidha amesema endapo atachaguliwa atakamilisha ahadi zilizoahidiwa na mtangulizi wake marehemu Kwandika.

“Nitatimiza ahadi zote zilizoahidiwa, nitaleta maji yatawafikia hadi nyumbani kwani nishazungumza na Rais Samia Suluhu Hassan  na amekubali, nitaleta umeme na  kutakuwa na  uhuru wa kufanya biashara katika wilaya hii,”amesema Cherehani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles