27 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara yataka wasanii kushirikiana na serikali

Jessca Victor, TUDARCo

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesema sanaa ni biashara kubwa na endapo wasanii  watashirikiana na Serikali sekta hiyo itazidi kukua

Kihage amezungumza hayo wakati akihutubia katika mkutano mkuu wa sekta ya sanaa  ambapo wadau na  wasanii wamewasilisha  changamoto zao kama vile bidhaa zinazotumiwa na wasanii kuwa na bei ambayo sio rafiki.

Amesema  lengo la mkutano huo ni  kujadili  sekta ya sanaa kati ya serikali na wadau  ili kufikia malengo ya  kufanya sekta hiyo kuendeshwa  kibiashara na kuleta tija.

“Wasanii ni masoko ya kutoka viwandani na pia ni wahamasishaji wa biashara mbalimbali kwa hutumika hata katika matangazo makubwa ya biashara nchini Tanzania na ulimwenguni kiujumla.

 “Wizara ya Viwanda na Biashara ni mdau mkubwa wa Wizara ya Sanaa na Utamaduni na Michezo, kwani sekta ya sanaa ni kiwanda kinachozalisha huduma za sanaa ambazo zinahitaji mchango mkubwa wa wizara,” amesema.

Ameeleza kuwa mipango ya Serikali ni kuweka mazingira wezeshi katika kukuza sanaa zetu ili kufikia kiwango cha Kimataifa, kuboresha mbinu za kimkakati ya utekelezaji wa sera na sheria za kurasimisha kazi na sanaa nchini na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sanaa hususani wasanii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles