27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Wasanii kukiwasha Dar Sunset Carnival

Jescar Victor, TUDARCo.

Wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva wanatarajiwa kutoa burudani katika tamasha la utalii la ‘Dar Sunset Carnival’ litakalofanyika Oktoba 3, mwaka huu kwenye fukwe za Coco, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe wakati wa kuzindua tamasha hilo, amesema  ni muendelezo wa kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Gondwe amesema tamasha hilo linasimamiwa na Mkuu wa Mkoa, Amosi Makalla katika kuhakikisha   fukwe zote zinakuwa safi na kuhamasisha  kukuza utalii wa ndani na nje.

Wananchi wakiwa Coco Beach katika moja ya sikukuu

Amewataja baadhi ya wasanii watakaotoa burudani siku hiyo kuwa ni Barnaba, Bell9, Mr Blue,Shoro Mwamba, Dully Sykes, G. Nako, vikundi vya ngoma na wengine wengi.

“Lengo ni kudumisha matumizi bora ya usafi katika fukwe ili kukuza utalii wa ndani na nje, huu ni mwanzo tu wa kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu, tunashukuru kwa wazo lake zuri”, amesema.

Pamoja na burudani amesema kutakuwa na uzinduzi wa gari la utalii, pia michezo ya watoto, hivyo kuwakaribisha wazazi kwenda kwa sababu usalama utakuwepo wa kutosha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles