JESTINA ZAUYA, TUDARCo
HOTUBA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Septemba 23,2021 katika mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imetajwa kuwa miongoni mwa hotuba saba muhimu zilizowahi kutolewa.
Hotuba hiyo imechaguliwa na tovuti ya Marekani ya ‘Foreign Policy [FP] kuwa ni miongoni mwa hotuba muhimu zaidi kutolewa kwenye kikao hicho huku ikiwa ni ya kipekee kutoka kwa mkuu wa nchi.
Katika mkutano huo, Rais Samia alihutubia kuhusu masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na janga la Uviko 19.
Viongozi wengine ambao hotuba zao zimeelezea mambo muhimu ni pamoja na Rais wa China  Xi Jinping, Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Lebanon Michel Aoun Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Rais wa Iran Ebrahim Raisi na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.