24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

UHURU, RAILA WAKUTANA KUMALIZA TOFAUTI ZAO

NAIROBI, KENYA


HATIMAYE Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amekutana na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo, Nasa na aliyekuwa mgombea wa urais, Raila Odinga, katika ofisi yake iliyopo ndani ya jengo la Harambee, jijini Nairobi.

Kukutana kwa viongozi hao kumesababisha mshtuko kwa baadhi ya wanasiasa na maelfu ya wananchi ambao wanataka kufahamu nini kilichozungumzwa nyuma ya pazia kabla ya kuitisha mkutano na vyombo vya habari huku wote wawili wakitoa hotuba ya kuwaunganisha Wakenya na kuijali nchi hiyo.

Viongozi hao wamekubaliana kuunda mpango wa pamoja wa utekelezaji wa malengo ya pamoja waliyokubaliana katika kikao chao ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku chache zijazo na kuongozwa na Balozi Martin Kimani kwa upande wa Rais Kenyatta, wakati upande wa Odinga, utaongozwa na Paul Mwangi.

Taarifa za Ikulu ya nchi hiyo kwa vyombo vya habari imesema kuwa majadiliano na makubaliano ya mpango huo yametiwa sahihi na viongozi wote wawili pamoja na kukubaliwa na kila upande juu ya kuanza utekelezaji.

Kenyatta na Odinga wamefanya mkutano huo muda mfupi kabla ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson, kuwasili nchini humo kwa ziara ya siku nne. Mara kadhaa Serikali ya Marekani imehimiza kufanyika kwa mazungumzo na mashauriano kutatua mzozo wa kisiasa uliokumba taifa hilo baada ya uchaguzi wa Agosti 8, mwaka jana.

Akitoa hotuba yake mbele ya vyombo vya habari baada ya kikao chake na Rais Kenyatta, Raila Odinga, amesema amekubaliana na rais wa nchi hiyo kuwa hekaheka za kisiasa zimefika kikomo na kwamba wamekataa kuwa watu ambao chini yao (Kenya) kuwa taifa lililofeli.

“Ndugu zangu Wakenya, uhai wa taifa lolote una muda ambao wananchi na viongozi wao wanatakiwa kurekebisha michakato ambayo itawapeleka katika mafanikio ya malengo yao na sala zao za kulinda nchi huzingatiwa. Abraham Lincoln, amewahi kusema kama tungetambua mahali tulipo na kuwa na utayari, tungekuwa na maamuzi mazuri juu ya nini cha kufanya na namna ya kutekeleza, muda kama huo unapofika, viongozi wanalazimika kuhakikisha wanalinda malengo; katika suala letu, haki, umoja, amani, uhuru na maendeleo kwa wote ni kazi yao. Muda huo umefika Kenya. miaka 54 ya uhuru, tumekuwa na changamoto ya kukagua mwelekeo wetu uliopiganiwa na babu zetu na kuanzisha taifa huru ambao walifariki wakiwa wazalendo.

 

Inaendelea……………. Jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles