25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 95 machinga Ilala wapata vitambulisho

AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa machinga Kariakoo Steven Lusinde, amesema asilimia 95 ya machinga katika Wilaya ya Ilala, wameshapewa vitambulisho vilivyozindulia na Rais John Magufuli kwa ajili ya watu wa kada hiyo.

Alisema awamu ya kwanza vitamvulisho vilivyotolewa vilikuwa 5,000 na awamu ya pili 27,000 ambapo jumla ya vitambulusho 32,000 vilitolewa kwa Wilaya ya Ilala huku bado kukiwa na uhitaji wa vitambulisho vingine. 

“Vitambulisho vimeisha, wamachinga waliopata ni asilimia 95 tu, tumeshatoa taarifa ili tutengenezewe vingine, vitakapofika zoezi litaendelea, nawashauri wamachinga wafate maelekezo ya mheshimiwa Rais ili kuchangia maendeleo ya nchi,”alisema Lusinde.

Lusinde alisema wamedhibiti watu wanaodanganya ili kupata vitambulisho kutokana na mfumo wa database walionao kwahiyo watu wote wakipewa vitambulisho hivyo ni halali. 

“Watu wengine wanadanganya kwaajili ya kupata vitambulisho, sisi tunadhibiti kwasababu tuna database pia tunawaripoti watu wanaojiingiza kupata vitambulisho ambao sio halali,”alieleza Lusinde.

Naye mmoja wa wamachinga, Mustaph Mashushanga, alisema vitambulisho walichopata vitawasaidia kuepuka usumbufu kwani wanauwezo wa kufanya biashara hata sehemu zingine. 

“Sasa hivi hatupati usumbufu kwani vi vitambulisho vimetusaidiq kutambulika popote kwahiyo tunafanya biashara kwa uhuru tofauti na zamani, nawashauri machinga wote wapate vitambulisho ili wafanye biashara kwa amani,”alieleza Mashushanga.

Aliongeza”pia naishauri serikali kuangalia na aina ya biashara ya may kuna wengine wanauza mihogo au kuna wengine wanafaya biashara ndogo zaidi ambao kupata kiasi cha 20000 ni nyingi kwao naomb  hawawaangaliwe.

Desemba mwaka jana,Rais John Pombe Magufuli akizindua vitambulisho 670,000 vya kukabidhiwa kwa wakuu wa mikoa kwaajili ya matumizi ya wajasiriamali wadogo wadogo  (machinga) katika Mikoa yote ya Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles