30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

TCRA yazifungia simu za wizi milioni 1.6

Na AZIZA MASOUD-Dar es Salaam

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezifungia simu 1,682,667 zilizokuwa zikitumika kwenye mitandao mbalimbali ambazo zilibainika kutokuwa na sifa zikiwamo kutofikia viwango vinavyotakiwa, zilizoibwa na zilizoripotiwa kupotea.

Takwimu hizo zitolewa jana na Mkurugenzi wa TCRA, James Kilaba wakati akiwasilisha taarifa juu utendaji kazi wa Mfumo wa Kuratibu  na Kusimamia Mawasiliano ya Simu(TTMS) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC)   waliotembelea ofisi za mamlaka hiyo.

Alisema  kasoro za simu hizo zimebainika kupitia mtambo wa TTMS ambao pamoja na mambo mengine ina  moduli ya CEIR(Central  Equipment Identifications Register) ambayo  ina kipengele cha kutambua taarifa za  laini za simu(sim card profile) na namba tambulishi za mawasiliano.

“Moduli ya CEIR  imewezesha kuzifungia simu 1,682,667 zilizokuwa zikitumika kwenye mitandao mbalimbali, idadi hii inajumuisha  simu zilizobainika  kutofikia viwango vinavyotakiwa, simu zilizonakiliwa namba tambulishi(IMEI) pamoja na zile zilizoropitiwa kuibwa ama kupotea,” alisema   Kilaba.

Alisema   mtambo huo pia umewezesha  kubaini mawasiliano ya simu za kimataifa zinazoingia kwa ulaghai ambako mpaka sasa  yamepungua na kufikia chini ya asilimia 10 kwa mwaka jana kutoka asilimia 65  mwaka 2013.

Alisema  mfumo huo umeonyesha  miamala ya  fedha iliyofanywa na  kampuni za simu ambayo imefikia  Sh bilioni 8.9 kutoka Novemba 2014 hadi Februari 2019 ilyozalisha faida ya Sh trilioni 2.5.

  Kilaba alisema mfumo huo pia unatoa takwimu za huduma za mawasiliano ya simu za sauti, matumizi ya data na ujumbe mfupi pamoja na fedha zinazopatikana katika kila kampuni ya simu kupitia miamala ya fedha na upigaji wa simu.

Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka  alisema  wamefurahishwa na utendaji kazi wa mfumo huo ambao unaonyesha uwazi  katika matumizi ya vifaa  mitandao  tofauti na ilivyo awali.

“Awali kulikuwa na malalamiko  mpaka miongoni mwa wabunge kuhusu upotevu wa fedha kutoka katika kampuni za ismu kwenda serikali.

“Mtambo huu umekuja kuondoa haya malalamiko kwa kuwa tumeona kuna uwazi mkubwa na teknolojia ni nzuri na ya kisasa,”alisema Kaboyoka.

Alisema utendaji kazi wa mfumo huo utaleta tija kwa kuongeza mapato ya serikali na  pato la taifa kwa ujumla kupitia mawasiliano ya simu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles