Picha zisizo na maadili mtandaoni zamponza Sister Fey

0
1097

Bethsheba  Wambura, Dar es Salaam

Jeshi la polisi nchini linamshikilia msanii wa muziki na filamu Faidha Omary maarufu Sister Fey kwa matumizi mabaya mitandao ya kijamii hususani Instagram Kutokana na kutuma picha mnato na nyongefu zisizokuwa na maadili.

Akithibitisha tukio hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram leo, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo  Juliana Shonza amesema kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wadau wa filamu na baadhi ya wananchi Serikali imemchukulia hatua msanii huyo na yuko chini ya ulinzi hadi uchunguzi utakapokamilika.

Amesema uchunguzi utakapokamilika msanii huyo atafikishwa mahakamani na kuwataka  Watanzania hasa wasanii kuzingatia sheria za matumizi ya mitandao.

“Napenda kutoa rai kwa Watanzania hasa wasanii kuzingatia sheria za mitandao ya kijamii na Serikali iko macho na haitosita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayekiuka maadili ya mtanzania,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here