Bethsheba Wambura, Dar es Salaam
Aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh amesema mivutano inayoendelea hivi sasa juu ya uwajibikaji wa CAG wa sasa Profesa Musa Assad ni ya kudhoofisa utendaji kazi wake na wala haina tija kwa nchi.
Akizungumza katika mahojiano yake na kituo cha redio cha BBC Utouhamesema Profesa Assad anatimiza wajibu wake kikatiba inayomtaka akimaliza utendaji wake ripoti ipelekwe bungeni kujadiliwa kama mfumo unavyoelekeza sasa kama anaotakiwa kufanya nao kazi ndiyo wanasema hawana imani nae hali hii inadhoofisha ufanyaji kazi.
Utoh amesema mfumo unaotumika hapa nchini hauumpi CAG mamlaka ya kusimamia na kutekeleza mapendekezo yake bali akifanya kazi yake inapelekwa bungeni ambalo ndilo litaelekeza nini serikali ikifanye.
Akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa BBC kuhusu kitabu chake cha ‘Uwajibikaji ndani ya kalamu isiyokuwa na wino’ na kile kinachoendelea sasa hivi kuhusu ripoti ya CAG, Utouh amesema alichokiandika humo kinaakisi kila kinachotokea hapa nchini hivi sasa.
“Kitabu hiki kina mambo yote yanayotokea hapa nchini ukisoma katika ukurasa wa tano unasema CAG anatembea katika kamba nyembamba na sura ya sita inazungumzia meno yanaposagika bila sababu na mambo yote haya yanatokea sasa hivi kuwa na mivutano isyokuwa na tija kwa nchi zaidi ya kudhoofisha utendaji kazi.
“Ofisi ya CAG ni jicho la wananchi na ndiyo sababu ripoti yake inapelekwa bungeni kwa wawakilishi wananchi na jana nilifurahi kuona ripoti yake imepelekwa bungeni na kuwekwa wazi,” amesema Utouh.
Aidha Utouh amesema ofisi ya CAG ni nyeti na ipo kikatiba na ndiyo maana hata Rais hana urahisi wa kumvua madaraka japo yeye ndiye humteua.