26.5 C
Dar es Salaam
Saturday, January 22, 2022

Ripoti ya CAG yamuibua Utouh


Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh amesema mivutano inayoendelea hivi sasa juu ya uwajibikaji wa CAG wa sasa Profesa Musa Assad ni ya kudhoofisa utendaji kazi wake na wala haina tija kwa nchi.

Akizungumza katika mahojiano yake na kituo cha redio cha BBC Utouhamesema Profesa Assad anatimiza wajibu wake kikatiba inayomtaka akimaliza utendaji wake ripoti ipelekwe bungeni kujadiliwa  kama mfumo unavyoelekeza sasa kama anaotakiwa kufanya nao kazi ndiyo wanasema hawana imani nae hali hii inadhoofisha ufanyaji kazi.

 Utoh amesema mfumo unaotumika hapa nchini hauumpi CAG mamlaka ya kusimamia na kutekeleza mapendekezo yake bali akifanya kazi yake inapelekwa bungeni ambalo  ndilo litaelekeza nini serikali ikifanye.

Akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa BBC kuhusu kitabu chake cha ‘Uwajibikaji ndani ya kalamu isiyokuwa na wino’ na kile kinachoendelea sasa hivi kuhusu ripoti ya CAG, Utouh amesema alichokiandika humo kinaakisi kila kinachotokea hapa nchini hivi sasa.

“Kitabu hiki kina mambo yote yanayotokea hapa nchini ukisoma katika ukurasa wa tano unasema CAG anatembea katika kamba nyembamba na sura ya sita inazungumzia meno yanaposagika bila sababu na mambo  yote haya yanatokea sasa hivi kuwa na mivutano isyokuwa na tija kwa nchi zaidi ya kudhoofisha utendaji kazi.

“Ofisi ya CAG ni jicho la wananchi na ndiyo sababu  ripoti yake inapelekwa bungeni kwa wawakilishi wananchi na jana nilifurahi kuona ripoti yake imepelekwa bungeni na kuwekwa wazi,” amesema  Utouh.

Aidha Utouh amesema ofisi ya CAG ni nyeti na  ipo kikatiba na ndiyo maana hata Rais hana urahisi wa kumvua madaraka japo yeye ndiye humteua.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,947FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles