23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Zidane akataa tena kazi United

MANCHESTER, England

KWA mara ya pili, kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amesema havutiwi na mpango wa kuchukua mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer pale Old Trafford.

Presha ya kutimuliwa imeendelea kumwandama Solskjaer, hasa baada ya kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Manchester City mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mbali ya Zidane, pia Man United walikuwa wakihusishwa na huduma ya kocha wa kimataifa wa Italia, Antonio Conte, lakini aliishia mikononi mwa mabosi wa Tottenham.

Mara zote Zidane mwenye umri wa miaka 49 amekuwa akisisitiza kuwa ni kazi ya kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa ndiyo anayoimezea mate.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles