27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Iniesta: Xavi kwenda Barca imekaa poa!

CATALUNYA, Hispania

KIUNGO wa zamani wa Barcelona, Andres Iniesta, amesifia hatua ya klabu hiyo kumpa ukocha lejendari mwenzake, Xavi.

Xavi (41), ambaye alikuwa akiinoa Al-Sadd ya Qatar, alimalizana na Barca wiki iliyopita kuchukua nafasi ya kocha raia wa Uholanzi, Ronald Koeman.

“Ameiva, amejiandaa na ana uwezo. Ni mtu sahihi kwa kweli. Si kwa sababu anaijua La Masia na klabu, bali ameiva kuifanya kazi hii,” amesema Iniesta.

Katika mechi 91 alizoiongoza Al-Sadd, Xavi alishinda 62 na kuipa mara moja taji la Ligi Kuu huko Uarabuni.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles