26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Martinez anukia Aston Villa

LONDON, England

ASTON Villa hawana kocha tangu walipomfukuza Dean Smith mwishoni mwa wiki iliyopita na sasa wanahusishwa na mkuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez.

Ukiacha Martinez, Villa wanahusishwa na kocha wa Rangers ya Scotland, Steven Gerrard, sambamba na Kasper Hjulmand anayeinoa timu ya taifa ya Denmark.

Juu ya Martinez, taarifa za kituo cha televisheni cha Sky Sports kimenyetisha kuwa mabosi wa Villa watakutana naye mezani siku chache zijazo.

Kwa upande wake, kocha huyo atakayekwenda na Ubelgiji kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwakani, ameonesha nia ya kufanya kazi England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles