27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Fei Toto, Nabi wabeba tuzo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

KOCHA Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ametwaa tuzo ya kocha bora wa Oktoba wa Ligi Kuu Tanzania Bara,huku nyota wake Feisal Salum ‘Fei Toto’, akichukua ya mchezaji bora.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu, Fei Toto alishindanishwa na wachezaji Ramadhan Chombo wa Biashara United na Fiston Mayele wa Yanga katika hatua ya fainali.

Upande wa kocha Nabi aliwashinda Mbwana Makatta wa Dodoma Jiji na Francis Baraza wa Kagera Sugar.

Aidha Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania,Malale Hamsini, ametwaa tuzo ya kocha bora wa Septemba na mshambuliaji wa timu hiyo, Vitalis Mayanga akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi huo.

Malale ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda Hemed Suleiman Alli ‘Morocco’ wa Namungo na Hererimana Haruna wa Mbeya Kwanza.

Mayanga amewashinda Obrey Chirwa wa Namungo na Clephas Mkandala wa Dodoma Jiji alioingia nao fainali.

Tuzo hizo zimetangazwa leo Novemba 8,2021 baada ya kikako cha Kamati ya Tuzo za TFF kilichokutana mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuwachagua wanamichezo hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles