24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mwigulu azitaka Halmashauri zilipokea mikopo kurudisha kwa wakati

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Mwigulu Nchemba amezitaka Halmashauri 55  zilizopokea mikopo ya fedha yenye thamani ya shilingi bilioni 50   kuhakikisha  wanazitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa na  kuzirudisha kwa wakati  ili halmashauri nyingine zipate fursa za kukopa. 

Akizungumza leo Novemba 8,2021,jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji saini ya makubaliano wa utoaji wa fedha za mikopo ya  utekelezaji wa programu ya kupanga ,kupima na kumilikisha ardhi nchini,Waziri huyo amezitaka halmashauri hizo kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Waziri Nchemba amesema  serikali imetoa kiasi cha sh bilioni 50 kwa halmashauri 55 nchini kupitia wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kusaidia upimaji wa ardhi kwenye maeneo yao.

Amesema  lengo la Serikali kutoa mikopo hiyo ni kuziwezesha Halmashauri hizo kupima ardhi ili kuondoa ujenzi holela kwenye maeneo hayo 

“Serikali itaendelea kutoa fedha hizo kutokana na hali ya bajeti itakavyokuwa imepangwa hivyo waliopata mikopo hiyo wanatakiwa kuonyesha mifano kwa wengine watakaohitaji,”amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeeo ya Makazi ,William Lukuvi amesema kupitia fedha hizo halmashauri zitaweza kutengeneza   bilioni 41 huku akitolea mfano Halmashauri ya Meru imekopa sh bilioni 1.6 na inatarajia kuingiza sh bilioni 7.8.

Waziri Lukuvi amesema  siku za nyuma Halmashauri zilikuwa zikiomba mikopo kutoka taasisi za kifedha lakini awamu hii serikali imechuku jukumu hilo.

Amesema  mikopo hiyo imetolewa na serikali kutokana na andiko lililoandikwa na Halmashauri husika kuhusu kazi za fedha hizo. 

Amesema  kuwa jumla ya Halmashauri 78 ziliomba mikopo hiyo lakini waliofanikiwa ni Halmashauri hizo 55 na watakuwa wakitoa mikopo hiyo.

Naye,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ameagiza mapato ya ndani ya maendeleo katika Halmashauri  kutumika pia katika  kupima na kupanga miji bila kutaja asilimia ambazo zinatakiwa kutengwa.

Hatua hiyo ilikuja kutokana na Waziri Lukuvi kumuomba Waziri Ummy Mwalimu Halmashuri zitenge fedha kidogo kwa ajili ya kupima na kupanga maeneo.

Waziri Ummy amesema kupatikana kwa fedha hizo kumeongeza vipaumbele alivyokusudia kwenye utendaji wake wa kazi alivyojiwekea wakati anaingi kwenye wizara hiyo.

Amevitaja  vipaumbele hivyo kuwa ni huduma za afya ,elimu msingi ,kuwawezesha wananchi kiuchumi hasa akinamama ,walemavu na vijana,ujenzi wa miundombinu ya barabara 

Waziri Mwalimu amesema  kwa sasa ameongezewe kipaumbele cha tano kilichongezewa hiyom jana kuwa ni upimaji ardhi kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

“Upatikanaji wa fedha hizo zitaenda kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi pamoja na Halmashauri husika,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles