27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Yemi Alade: Wasanii wajiheshimu jukwaani

Yemi-AladeLAGOS, NIGERIA

MSANII anayetamba na wimbo wake wa ‘Na Gode’ Yemi Alade, amesema wasanii wengi wa kike wanapenda kupanda jukwaani huku wakiwa na mavazi ya kitamaduni ya barani Ulaya.

Msanii huyo amedai kwamba kwa upande wake amekuwa tofauti sana na wasanii wengine wa barani Afrika, ambao wanapanda jukwaani huku wakiwa na mavazi yenye muonekano wa wasanii wa bara la Ulaya.

“Nikipanda jukwaani nakuwa tofauti na wasanii wengine hapa Afrika, siwezi kubadilika na kuvaa mavazi kama sio mtu kutoka Afrika, ningependa kuwaona wasanii wenzangu wakibadilika na kutangaza utamaduni wao hasa katika mavazi.

“Ninaamini tamaduni zetu zinaweza kuwa kivutio kwa mataifa mengine hasa ya bara la Ulaya na kikubwa ni kujituma katika kazi yako na sio kuiga mavazi,” alisema Yemi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles