Wema Sepetu kupamba Miss Iringa leo

Wemaaaaa....NA RAYMOND MINJA, IRINGA

MISS Tanzania 2006, Wema Sepetu, anatarajiwa kupamba fainali ya shindano la kumsaka mlibwende atakayeuwakilisha Mkoa wa Iringa katika shindano la Miss Tanzania mwaka huu.

Shindano hilo linafanyika katika Ukumbi wa Kichangani na mgeni rasmi ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.

Mwandaaji wa shindano hilo, Maya Said, akijitapa kama alivyowahi kujitapa Mkuu wa Wilaya hiyo, kwamba Miss Tanzania 2016 lazima atatoka katika mkoa huo kwa kuwa wana vigezo vya ziada.

Maya alisema lengo la shindano hilo ni kuutangaza Mkoa wa Iringa sambamba na kauli mbiu ya usafi wa mazingira na utalii wa ndani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here