22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA YALIA KUHUJUMIWA

Yataka Manara aadhibiwe

Na MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

SIKU moja baada ya wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kampuni ya Vodacom kukabidhi vifaa kwa timu 16, uongozi wa Yanga umelijia juu  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPB) kwa kuihujumu klabu yao kutokana na kutowapa taarifa kuhusu zoezi hilo.

 

Vodacom ilikabidhi vifaa hivyo jijini Dar es Salaam juzi ambavyo vitatumiwa na timu 16 zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao utakaoanza Agosti 26, mwaka huu.

 

Katika tukio hilo, Yanga haikuwa na mwakilishi hatua iliyomfanya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, kujitokeza na kuomba akabidhiwe kwa niaba ya watani zake hao.

 

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa kitendo cha jezi zao kutambulishwa bila wao kuwepo, kimehujumu mapato ya klabu yao kwavile tayari walishapanga siku ya kufanya hivyo kwa mashabiki wao.

 

“Yanga imeshangaa kuona jezi hizo zinatoka Vodacom wakati sisi tunajua Sportpesa ilimpa tenda Kassim Dewji ya kuweka nembo ya mdhamini.

“Utambulishaji wa jezi za Yanga uliofanywa na Vodacom jana (juzi) ni hujuma, kwa sababu kitendo hicho kimetupotezea mapato makubwa, kwani kama klabu tulipanga siku rasmi ya kuitambulisha jezi ya msimu ujao kwa mashabiki wetu ili kupata mapato,” alisema Mkemi.

“Tulipanga jezi zetu zitambulishwe na Sol Campbell (beki wa zamani wa Arsenal) ambaye amealikwa na wadhamini wetu Sportpesa.”

“Tutakaa na wanasheria wetu na kushauriana ili kuangalia namna ya kufungua kesi dhidi ya TFF) Bodi ya Ligi ya Vodacom.

“Yanga itapambana na yeyote atakayethubutu kuhujumu mapato yetu kupitia nembo ya klabu na hatutasita kuchukua hatua.”

 Manara kupokea jezi

Mkemi alizungumzia kitendo cha Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, kujitokeza na kupokea vifaa vya Yanga kwa kuitaka mamlaka inayohusika kumchukulia hatua za kinidhamu.

“Kwanini Manara achukue vifaa vyetu, mbona wakati wa utoaji wa tuzo za Vodacom, Mlimani City, Simba hawakuwa na mwakilishi lakini hakuna kiongozi wa Yanga aliyejitokeza, tunaomba wenye mamlaka wachukue hatua.

 

“Pia tunaiomba Bodi ya Ligi ituombe radhi kutokana na tukiO

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles