22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA YAREJEA KISHUJAA

Na MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wanarejea nchini leo kutoka Afrika Kusini, huku kocha wa timu hiyo, Joseph  Omog, akitamba kuwa ana kikosi chenye uwezo wa kupata matokeo mazuri dhidi ya mpinzani wake yoyote.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi jana, Omog alisema ameridhishwa na viwango vya wachezaji wake wapya pamoja na wale wa zamani baada ya kuwashuhudiwa wakifanya mambo makubwa katika michezo miwili ya kirafiki.

Ikiwa Afrika Kusini Simba ilicheza mchezo wake wa kwanza kirafiki Jumanne dhidi vigogo wa soka nchini humo, Orlando Pirates na kuchapwa bao 1-0 kabla ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na Bidvest Wits katika mchezo uliofuata.

 

“Nimevutiwa na uwezo wa kila mchezaji  katika kikosi changu, kila mmoja amejituma kuonyesha uhodari wake, ni jambo zuri kwa timu kwa ajili ya kuhakikisha tunafanya vizuri msimu ujao.

 

“Kwa aina ya wachezaji nilionao naamini tuna uwezo wa kupata matokeo mazuri dhidi ya mpinzani yeyote,” alisema kocha huyo wa zamani wa Azam FC.

 

Baada ya kurejea nchini, kikosi cha Simba kitaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wa siku maalumu wa  klabu hiyo ‘Simba day’ dhidi ya Rayon Sports, utakaofanyika Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Wekundu hao pia watashuka dimbani Agosti 23, kuumana na Yanga katika pambano la Ngao ya Jamii kushiriki ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Agosti 28, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles