27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA MAKENGEZA MMEYAPATA  WAPI?

NA ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


yngNIMEKUWA nikijiuliza kwa muda mrefu sana tangu dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza lilipofunguliwa Novemba 15, mwaka huu kuhusu utaratibu wa klabu ya soka ya Yanga  kujitekenya na kucheka yenyewe bila majibu.

Yanga siku hizi wamekuja na aina mpya ya utaratibu wa kusajili ambao haujawahi kuwapo hapo kabla, kuhusu kuficha wachezaji au makocha wanaotaka kuwasajili, jambo ambalo linawafanya kuishi kama digidigi kwa kuogopa kuonekana na vyombo vya habari au wapenzi na mashabiki wao wa soka nchini.

Huenda sababu pekee zinazowafanya kuogopa na kuamua kujificha zinatokana na kusajili wachezaji wengi vilaza na ubora usiolingana na klabu hiyo, huku mashabiki na wanachama wao wakiwabeza kushindwa kuwa na machaguo mazuri na sahihi linapokuja suala la kutafuta wachezaji wa kigeni wenye uwezo na vipaji.

Klabu hiyo hivi karibuni wamesajili kocha mpya Mzambia, George Lwandamina kimya kimya, mara kocha msaidizi Noel Mwandila kimya kimya, pia na kiungo mkata umeme Justine kimya kimya utadhni wana ugomvi na waandishi wa habari au walikutwa na tuhuma za wizi wa wachezaji.

Utaratibu huo unapatikana Barani Afrika tu katika nchi ambazo soka lake linaendeshwa kijanja kama Tanzania.

Katika soka la Ulaya kila klabu kuanzia kuitaka saini ya mchezaji fulani hadi kumsajili ikiwa pamoja na mshahara wake pamoja na fedha za usajili huwa hadharani, jambo ambalo kwetu alitakaa litokee abadani.

Sababu kubwa ya klabu ya Yanga na nyingine kama Simba na Azam FC kufanya usajili wa siri ni ishara ya kutokujiamini na aina ya wachezaji ambao mara kadhaa wamekuwa wakiwasajili kwa kushindwa kufuata vigezo na uwezo wa mchezaji husika.

Klabu hizo mara nyingine huitwa zoa zoa kwa kukusanya wachezaji ambao wengine walishaacha hata kucheza mpira ili mradi zionekane zimesajili wachezaji wa kigeni wenye majina makubwa.

Wapo ambao wanadai kuwa klabu hizo zimekuwa zikifanya usajili kwa kukurupuka bila kufuata vigezo au ndio ile 10%   inayopatikana kijanja.

Simba, Yanga na Azam FC kinachotokea hadi kuanza kujificha katika usajili wao ni rekodi zao za usajili wa wachezaji vilaza ambao wamekuwa wakibezwa na wanachama na mashabiki wao wa soka nchini.

Binafsi utaratibu huo kwa klabu hizo naona kama hauna tofauti na ule wa huendeshaji wa kijiwe cha kahawa ambao unafanywa kwa manufaa ya kikundi fulani, si vinginevyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles