24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kuiwinda Simba Ligi Kuu

YangaSimbaNA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara timu ya Yanga, leo itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuikaribisha timu ya Mtibwa Sugar.

Iwapo Yanga iliyo nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 56 itaifunga Mtibwa katika mchezo huo, itakalia usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 59 na hivyo kuishusha Simba inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 57.

Mechi ya mzunguko wa kwanza Mtibwa Sugar ilikubali kuwa mteja mbele ya Yanga kwa kufungwa mabao 2-0 katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Mtibwa iliyo nafasi ya nne ikiwa na pointi 42 ni timu ngumu kwa Yanga kutokana na kocha wake mzawa, Mecky Mexime, kuwafahamu vema Yanga.

Mbali na mchezo huo, mechi nyingine itakuwa katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, Coastal Union itakapoikaribisha JKT Ruvu.

Coastal ambayo hivi sasa inaonekana kuja kwa kasi hasa baada ya kurejea kwa mdhamini wao, Binslum, watahitaji ushindi ili waweze kujinusuru katika hatari ya kushuka daraja.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Ally Jangalu, hivi sasa kipo mkiani mwa msimamo wa ligi kikiwa na pointi 19 wakiwa wameshacheza michezo 26 wakati JKT Ruvu chini ya Abdallah Kibadeni imecheza mechi 24 na wamejikusanyia pointi 24 kibindoni wakiwa nafasi ya 13.

Ndanda FC itawakaribisha Kagera Sugar katika Uwanja wa Nangwanda Sijaoni mkoani Mtwara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles