26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli kuzindua ‘flyover’ za Tazara leo

pic+magufuliNa Faraja Masinde, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli, leo anatarajiwa kuzindua mradi wa uboreshaji wa barabara ya juu ‘flyover’ katika eneo la  Tazara jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), ilieleza kwamba hatua ya kuzinduliwa kwa mradi huo utasaidia kupunguza tatizo kubwa la msongamano wa magari katika jiji hilo.

“Kulingana na makadirio ya Ofisi za Takwimu Tanzania, jumla ya shilingi za Kitanzania bilioni 411.55 zilipotea katika mwaka wa 2013 pekee kutokana na msongamano huu. Na ujenzi wake unategemea kukamilika mnamo Oktoba, mwaka 2018.

“Ikiwa ni barabara ya kwanza ya juu nchini, barabara hii itakua ni alama ya kudumu katika ufunguzi wa zama mpya za mahusiano ya Tanzania na Japan. Pia itachangia uboreshaji wa maisha ya wakazi wa Dar es Salaam na ukuaji wa uchumi sio tu kwa Tanzania bali pia kwa nchi za jirani ambazo hazina bandari, zilizounganishwa na barabara ya Ukanda wa Kati,” ilieleza taarifa hiyo.

Mkataba wa ujenzi kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ulisainiwa Oktoba 15, mwaka jana na kushuhudiwa na Dk. Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi wa wakati huo.

Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (JICA), ina historia ya zaidi ya miaka thelathini sasa katika kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji jijini Dar es Salaam, ikiwemo na ujenzi wa Daraja la Salender mnamo mwaka 1980.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles