27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Waamuzi waibana TFF

tffNA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

KAMATI ya Waamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema kuwa haikubaliani na maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya kuwasimamisha waamuzi waliochezesha mechi za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza kati ya JKT Kanembwa FC dhidi ya Geita Gold na Polisi Tabora dhidi ya JKT Oljoro.

Pia kamati hiyo ipo tayari kuwasaidia waamuzi hao waliosimamishwa wakituhumiwa kupanga matokeo iwapo watakuwa tayari kukata rufaa.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Chama, alisema kuwa wakati suala hilo likifanyiwa uchunguzi na Kamati ya Nidhamu, hakuna mwamuzi yeyote mkongwe au aliyekuwepo katika kamati yao aliyeitwa ili kutafsiri mipaka na kanuni za kazi zao.

Alisema wao kamati ya waamuzi wamekuja kusikia maamuzi yakitolewa pasipo kushirikishwa jambo ambalo halipo kisheria lakini pia maamuzi yaliyotolewa hayakuwa na haki kwani hakuna ushahidi wa kutosha uliowakamatisha waamuzi hao.

“Kuanzia mwanzo hadi mwisho wa sakata lile hakuna aliyeshirikishwa katika kamati yetu, jambo ambalo kwa upande fulani si haki kwani na sisi tuna sheria na kanuni zetu ambazo tunazitumia uwanjani, lakini pia hadi hivi sasa hakuna ushahidi wa kutosha ni vipi wamekutwa na tuhuma za upangaji matokeo.

“Sisi kamati ya waamuzi, tupo tayari kuwasimamia bega kwa bega  iwapo kama wenyewe wanaona hawakutendewa haki na wakakata rufaa, lakini wakiomba tuwasimamie katika hilo tupo tayari,” alisema Chama.

Hivi karibuni Kamati ya Nidhamu ya TFF chini ya Makamu Mwenyekiti wake Wakili, Jerome Msemwa, iliwafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi wa mchezo kati ya JKT Kanembwa FC v Geita Gold, Saleh Mang’ola, kamisaa wa mchezo huo, Moshi Juma pamoja na mwamuzi wa mchezo kati ya Polisi Tabora dhidi ya JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi wa akiba, Fedian Machunde, waliofungiwa kwa muda wa miaka kumi  pamoja na kutozwa faini ya shilingi milioni kumi kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo kwenye michezo hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles