24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

WIZKID KUPIGA ‘SHOO’ BURE NIGERIA 

LAGOS, NIGERIA


MKALI wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, amesema anatarajia kulipa fadhila kwa mashabiki wake nchini humo kwa kupiga shoo bure.


Msanii huyo amepanga kuifanya shoo hiyo hivi karibuni, mjini Lagos, huku akidai kuwa, ni sehemu ya shukrani zake kwa mashabiki wanaomsapoti katika muziki wake.


“Nashukuru Mungu kwa sasa nimekuwa na mafanikio makubwa katika muziki wangu, ninaamini hii ni kutokana na kujituma kwangu pamoja na sapoti kutoka kwa mashabiki, hivyo lengo langu ni kuja kulipa fadhila kwa mashabiki nchini Nigeria kwa kuwapa shoo ya bure hivi karibuni,” alieleza Wizkid.


Hata hivyo, kutokana na kauli hiyo ya Wizkid, baadhi ya mashabiki wameonekana kuipinga, huku wakidai kuwa msanii huyo siku hizi hana muda wa kuishi nchini humo, muda mwingi yupo Marekani, hivyo hawezi kupiga shoo ya bure.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles