26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

DAVIDO KUOKOA MAISHA YA SHABIKI WAKE

LAGOS, NIGERIA


WIKI chache baada ya shabiki wa msanii wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke (Davido), Chiamaka Okeke kutangaza kujiua ifikapo Agosti 13 ambayo ni siku yake ya kuzaliwa endapo hatakutana na Davido, ni bahati kwamba Davido amekubali kukutana na shabiki huyo siku yake ya kuzaliwa.

Davido amesema yupo tayari kuhudhuria siku hiyo ya kuzaliwa kwa shabiki yake huyo ili kuweza kuokoa maisha yake baada ya kuona malalamiko ya shabiki wake huyo aliyesema tangu 2014, alijaribu kutuma ujumbe, lakini hakufanikiwa kujibiwa wala kukutana naye.

“Wiki chache zilizopita kulikuwa na video ya shabiki wangu akitangaza kujiua kutokana na kunitafuta kwa muda mrefu bila mafanikio ya kuniona, hivyo sipo tayari kusababisha kifo chake, nitahakikisha nahudhuria siku hiyo ya kuzaliwa kwake ili niokoe maisha yake,” aliandika Davido kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,371FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles