24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

WIZKID HATAKI KUSIKIA SIASA

LAGOS, NIGERIA

IKIWA baadhi ya wasanii wanakimbilia kwenye siasa na kufanikiwa, mkali wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, amewaambia mashabiki zake kwamba hana mpango wa kuingia kwenye siasa.

Baadhi ya mashabiki walitumia mitandao ya kijamii, huku wakitaka siku moja aje kuingia kwenye mambo ya siasa, hivyo amewajibu kwa kusema Serikali ya Nigeria haitaki mchezo hivyo hawezi kuwa mwanasiasa.

“Ni kweli kuna wakati nilikuwa nafikiria siku moja nije kuingia kwenye siasa, lakini naomba niweke wazi kwamba haiwezekani kwa upande wangu, Serikali ya Nigeria haitaki mchezo hivyo ninaogopa kuingia kwenye matatizo.

“Wapo ambao wanapenda siasa kama nilivyo mimi kwenye muziki, hivyo itakuwa ngumu kuweza kunibadilisha kwa kile ninachokiamini kwa Serikali ya Nigeria, nitaendelea kufanya muziki hadi mwisho wa maisha yangu,” alijibu Wizkid.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles