26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

WAKALI DANCERS WAFUNIKA MIAKA 40 YA SAFARI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAM

WASANII wa kundi la Wakali Dancers wenye makazi yao Temeke, mwishoni mwa wiki walitoa burudani ya aina yake katika Tamasha la miaka 40 ya Bia ya Safari lililofanyika katika Ukumbi wa Bulyaga Park.

Tamasha hilo ni mwendelezo wa tamasha kubwa lililofanyika viwanja vya Leaders Club, lenye lengo la kufurahi na wateja wa Bia ya Safari inayoadhimisha miaka 40 tangu kuanza kutengenezwa kwake.

Pamoja na wasanii hao, pia kulikuwa na wasanii wengine kama Dully Sykes, Joh Makini na Juma Nature ambao pia walikonga nyoyo za mashabiki wa Temeke.

Meneja wa Bia ya Safari, Edith Bebwa, alisema hatua ya mafanikio iliyofikiwa na bia hiyo ni ya kujivunia na hasa kwa sababu bado inaendelea kuwa moja ya kinywaji kinachopendwa zaidi katika soko lenye chapa nyingi za bia.

“Tunajivunia kuwa nchini kwa miaka 40 na tunawaalika wateja wetu wote na wapenzi wa Safari Lager waje kusherehekea pamoja nasi wajivunie na wao kwa hatua hii ya mafanikio kwa sababu wao ndio wadau wetu wakubwa,” alisema Edith.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles