MARTIN MAZUGWA NA MITANDAO
UNAPOTAJA makocha wenye heshima kubwa katika ardhi ya Uingereza na duniani kwa ujumla, huwezi kulikosa jina la Mfaransa, Arsene Wenger kocha wa washika bunduki wa London Kaskazini, ambaye ndiye kocha aliyeweka rekodi ya kudumu katika kikosi hicho kwa muda mrefu.
Wenger amefikisha miaka 21 akikiongoza kikosi cha Arsenal tangu alipokabidhiwa timu, mara baada ya kuondoka kwa kocha Bruce Rioch, akiwa ametoka kuzifundisha Nancy, Monaco za ufaransa pamoja na Nagoya Grampus Eight ya Japana.
Ndani ya miaka 21 hiyo aliyokaa katika kikosi hicho akianzia uwanja wa Highbury, kisha Fly Emirates, amefanikiwa kubeba mataji, 16 huku akiwa ametumia kiasi cha Trilioni 2 akiwa kocha mwenye mafanikio zaidi kuwahi kufundisha klabu hiyo.
Misimu ya karibuni kocha huyo ameanza kupata joto ya jiwe kutoka kwa mashabiki wanaomtaka kuachana na timu hiyo, mara baada ya kukiongoza kikosi miaka 13 mfululizo pasipo kutwaa taji la Ligi Kuu.
Haya ni baadhi ya mambo ambayo yamempa heshima Wenger.
Kikosi cha dhahabu cha msimu wa 2003/04 kilichocheza michezo 49 pasipo kupoteza, rekodi ambayo ameshindwa kuivunja tena.
Wenger ambaye tangu aanze kukinoa kikosi hicho amecheza michezo 790 akiwa ameshinda michezo 457 na kutoa sare 193, huku akiwa amepoteza michezo 140 pekee.
Katika miaka 21 aliyokiongoza kikosi cha washika mitutu wa London miaka 20, amemaliza akiwa ndani ya nne bora huku mwaka 21 akianza kwa kuondolewa katika nafasi nne za juu.
Katika kipindi hicho alichokaa katika kikosi cha Arsenal, klabu kubwa za Chelsea, Liverpool, Manchester City pamoja na Manchester United tayari zimebadili makocha 42, huku Mfaransa huyo akisalia na kibarua chake.
Rekodi mbovu katika fainali za Ulaya
Wenger ambaye ameshinda jumla ya fainali 12 za mashindano tofauti, amekuwa na rekodi isiyovutia katika fainali za Ulaya ambapo kwenye mashindano ya Uefa Cup mwaka 2000, alipoteza kwa matuta mbele ya Galatasaray kwa mikwaju ya penati 4-1.
Huku pia akipoteza mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwaka 2006 mbele ya Barcelona, mara baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1.
Totenham Hortspurs waweka rekodi
Kumaliza msimu uliopita nje ya nne bora hii ni mara ya kwanza, lakini pia ni mara ya kwa washika mitutu hao wa London Kaskazini kumaliza chini ya mahasimu wao wa jiji moja spurs katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.
“Moja kati ya vitu vilivyowachanganya mashabiki kuhusu uwanja mpya kushindwa kuwapa kile walichokitarajia, mara baada ya kutoka Highbury.
“Nilipoondoka mwaka 2004 nilijisikia vibaya. Kwani tulitoka katika kipindi kizuri cha kushinda michezo yote pasipo kupoteza,” alisema Keown.