27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa JK aukwaa uenyekiti Chadema

Dk. Makongoro MahangaNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

ALIYEKUWA kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Ilala.

Dk. Mahanga, ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, alichaguliwa jana na Baraza Ushauri Mkoa wa Ilala.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa Dk. Mahanga, alisema kuwa anawashuku wana Chadema wenzake kwa mwamini kushika nafasi hiyo ya uongozi.

“Nawashukuru sana viongozi wa Chadema ngazi ya jimbo la Segerea na Mkoa wa Ilala kwa kuniamini kwenye Uongozi. Baada ya kuteuliwa na kupitishwa na Kamati Tendaji jimbo la Segerea kuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya jimbo Aprili 2016,  leo  (jana), wajumbe wa Baraza la Ushauri Mkoa wa Ilala wamenichagua kwa kura za kishindo kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ilala.

“Nawaahidi viongozi na wanachama wa Chadema Mkoa wa Ilala uongozi uliotukuka katika kukiimarisha na kukijenga Chama chetu katika mkoa wetu wa Ilala,” alisema Dk. Mahanga.

Agosti 2, mwaka jana Dk. Mahanga pamoja na makada wezake 20 waliokuwa wanaCCM walitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema .

Wakati akitangaza kuihama CCM , Dk. Mahanga, alisema anahamia Chadema kutokana na kutokuwepo demokrasia ya kweli.

Kwa miaka mingi Mahanga amekuwa akitajwa kama mwanasiasa kijana ambaye ni mfuasi mkubwa wa Lowassa, na ilitazamiwa kuwa hatabaki CCM iwapo ataangushwa katika kura za maoni za kuwania tena ubunge.

Inasemekana kuwa kwake mtiifu kwa Lowassa kumemchongea.

“Ninatangaza rasmi kuwa kuanzia leo tarehe 2 Agosti 2015, mimi Makongoro Mahanga si mwanachama tena wa CCM na ninakusudia kujiunga Chadema kama kitakubali kunipokea,” alisema Mahanga mbele ya wanahabari

Mahanga ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kazi, alitoa tamko hilo saa chache baada ya kuthibitika rasmi kuwa ameangushwa katika kura za maoni za kutafuta mgombea wa CCM kugombea ubunge jimbo hilo.

Katika hali iliyoonesha ukubwa wa tatizo la uchafuzi wa taratibu linalolaumiwa kukithiri ndani ya mfumo wa CCM, Mahanga alisema amechukizwa na wizi wa kura uliofanywa wakati wa uchaguzi huo.

“Nawataka pia wanachama wengine wa CCM ambao hawakufurahishwa na wizi wa kura uliofanyika, waungane nami kujiunga na Chadema,”  alisema mbele ya waandishi wa habari aliokutana nao nyumbani kwake, Plot 1071, Kitalu S, Segerea mwisho, Dar es Salaam.

Matokeo yaliyomuangusha Mahanga, ni muendelezo wa vipigo vilivyowakumba viongozi maarufu wa CCM katika kura za maoni zilizofanyika nchini kote jana, wakiwemo mawaziri serikalini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles