30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa Jaji Bomani apewa nafasi nyeti UDP

Jaji Mark BomaniJOHANES RESPICHIUS, DAR ES SALAAM

CHAMA cha United Democratic (UDP) kimemteua, Andrew Bomani, kuwa Mkurugenzi wa Mikakati  na Mambo ya Nje ya chama hicho.

Mbali na kupewa nafasi hiyo pia chama hicho kimemteua kuwa Kaimu Katibu Mwenezi.

Andrew ni mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu , Jaji Mark Bomani, ambaye aliteuliwa na kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Juni 18, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana  Mwenyekiti wa UDP,  John Cheyo, alisema pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu pia ilimteua Dk. Goodluck ole Medeye, kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho.

Ole Medeye ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwishoni mwa mwaka jana na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kabla ya kuhamia UDP.

“Jana (juzi) Kamati Kuu ya chama ilikaa kikao maalumu kwa ajili ya mambo makuu mawili ambayo ni pamoja na kufanya uteuzi wa nafasi mbili ya Kaimu Katibu Mkuu wa chama na nafasi tuliyoiunda mahususi ya mkurugenzi wa mikakati ya chama na mambo ya nje.

Wajumbe wa kamati walikubaliana kwa pamoja na  kumteua Dk. Goodluck ole Medeye kuwa Kaimu Katibu Mkuu na Andrew kuwa Mkurugenzi wa Mikakati ya chama na Mambo ya Nje lakini pia Kaimu Katibu Mwenezi,” alisema Cheyo.

Aliwataka viongozi hao wapya kutofanya siasa za kuwatukana watu wala Serikali iliyopo madarakani bali waweke utaifa mbele kwa faida ya Watanzania wote.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa UDP, Dk Medeye, alisema kitendo cha Serikali kuendelea kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa kwa kisingizio cha sababu za kiintelejensia kinalenga kudumaza vyama.

“Kama hali hii itaendelea nchini tunaelekea kurudi kwenye siasa za chama kimoja ambayo tuliziacha mwaka 1992 hivyo namuomba Rais Dk. John Magufuli aingilie kati suala hili na kuruhusu vyama vya siasa viendele na mikutano yake,” alisema Medeye.

Medeye ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Serikali ya awamu ya nchi chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuitisha mkutano wa vyama vyote ilikijadili misingi ya nchi kutokana na hali na marufuku hiyo ya Jeshi la Polisi kufanya mikutano ya vyama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles