22.9 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa afya ataka mpango mkakati kusimamia usafi

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ameitaka Idara ya Kinga Wizara ya Afya kuimarisha mpango mkakati wa kusimamia suala la usafi wa mazingira katika majiji makubwa pamoja na maeneo ya mipakani mwa nchi.

Waziri Mhagama amesema hayo leo Septemba 9, 2024 wakati wa kikao na Idara ya Kinga Wizara ya Afya kwa lengo la kujadiliana utendaji kazi wa idara hiyo pamoja na kujua majukumu ya Idara hiyo.

“Tukumbushane kuzingatia usafi, kuanzia katika mikoa mikubwa (majiji) kama vile mkoa wa Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza pamoja na mipakani hii itaweza kusaidia mikoa mingine kuiga mfano huu na hatamaye tutafanikiwa nchi nzima.” Amesema Waziri Mhagama.

Aidha ameelekeza kuwa kutengenezwa kwa programu maalum ya kusimamia suala la matumzi ya vyoo bora na kutumika kwa ufasaha ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko na kuleta usalama wa Afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga Dk. Ntuli Kapologwe wakati akiwasilisha taarifa yake amesema, afya ya mazingira inajumuisha afua zinazolenga kuzuia visababishi vya magonjwa ambapo afua hizo ni pamoja na usafi wa mazingira, udhibiti wa wadudu wadhurifu na wanyama waharibifu.

“Lakini pia afua nyingine ni pamoja na udhibiti wa taka, usalama wa chakula, usalama wa maji ya kunywa, udhibiti wa magonjwa mipakani, huduma za Afya mahala pa kazi pamoja na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira.” Amesema Dk. Ntuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles