22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Bashungwa,Ndejembi wakutana na Mtendaji Mkuu wa K-FINCO

Na Mwandishi wa Wizara

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akiwa ameambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi wamekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fedha ya Korea kwa ajili ya Ujenzi (K-FINCO)Dk. Lee Eun Jae pamoja na watendaji wakuu wa kampuni za ujenzi zaidi ya 30 ya Korea Kusini.

Katika Mazungumzo yaliyofanyika katika nyakati tofauti,Bashungwa amewasilisha mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kuwezesha Makandarasi Wazawa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo ameyakaribisha makampuni ya Korea kufika nchini na kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na ujenzi wa nyumba za makazi na biashara.

Bashungwa ametoa wito kwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya K-FINCO kuyawezesha Makampuni ya Ujenzi ya Korea kushirikiana na Makandarasi Wazawa katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi nchini Tanzania ambayo yatawezesha wazawa kujengewa uwezo na kupata ujuzi wa teknologia za ujenzi wa miundombinu.

Aidha, Bashungwa ameeleza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Tanzania katika sekta ya miundombinu ikiwa ni pamoja na Korea kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za ‘expressway’ na kutekeleza miradi ya kupunguza msongamano katika majiji kwa utaratibu wa PPP, na kuunganisha mtandao wa barabara na nchi za EAC na SADC.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu (K-FINCO), Dk. Lee Eun Jae ameeleza kuwa Serikali ya Korea itaendelea kushirikiana na Tanzania ambapo tayari wameshafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na kusaini hati za makubaliano na Wizara ya Ujenzi na taasisi mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB.

Mawaziri hao wakiwa na mwenyeji wao, Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Togolani Mavura wanaendelea na ziara ya kikazi nchini Korea Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles