30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mulamula ziarani Finland

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amewasili nchini Finland kwa ziara ya siku 3 kushiriki mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nchi za Nordic (NORDIC-AFRICA) unaofanyika kuanzia Juni 13 hadi 15, 2022 jijini Helsinki, Finland.

Mkutano huo umeanza na hafla ya ufunguzi iliyofanyika leo Juni 13, 2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Pekka Haavisto.

Akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo, Haavisto alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika kujiletea maendeleo baina ya nchi hizo marafiki.

Aidha, mkutano huu utahusisha nchi 5 za Nordic ambazo ni Finland mwenyeji wa mkutano wa sasa, Sweden, Norway, Iceland na Denmark na nchi za Afrika 25 marafiki wa Nordic.

Mkutano huo wa Mawaziri wa Mambo ya Nje utahusisha Mabalozi wa nchi shiriki za Afrika zinazowakilisha katika nchi za Nordic na Mabalozi wa nchi za Nordic wanaowakilisha katika nchi shiriki za Afrika.

Wazo la kuanzisha mkutano huu lilianza mwaka 2000 ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika nchini Sweden mwaka 2001. Baada ya hapo mikutano kama hii inafanyika kwa kupokezana kutoka Bara la Afrika na upande wa Nordic.

Mwaka 2019 Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano huu ambapo nchi takribani 34 zilishiriki katika mkutano.

Wakati huo huo Mhe. Waziri Mulamula ametumia fursa ya ziara hiyo kutembelea Makao Makuu ya Ofisi ya Mpango wa usimamizi wa migogoro nchini Finland na kukutana na uongozi wa mpango huo. Lengo la likiwa kujadili masuala ya amani na usalama katika ukanda wa Afrika Mashariki na ukanda wa kusini mwa Afrika.

Katika mazungumzo yake Waziri Mulamula ameeleza kuwa Tanzania inaendelea kuwa mstari wa mbele katika kusimamia masuala ya amani na usalama ili kuwezesha nchi za ukanda huo kufanya shughuli za kiuchumi na kuinua maendeleo ya taifa na wananchi kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles