27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maafisa Kilimo Bariadi wapewa angilizo matumizi ya pikipiki

Na Derick Milton, Bariadi

Maafisa kilimo wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu wamepewa angalizo juu ya matumizi sahihi ya pikipiki zilizotolewa na Wizara ya Kilimo kuhakikisha zinakwenda kuongeza uzalishaji wenye tija kwenye katika mazao mbalimbali ya wakulima.

Sambamba na hilo wametakiwa kutozitumia katika matumizi binafsi ya starehe kama kwenye vilabu vya pombe, kubeba abiria (Bodaboda) ikiwemo matumzi mengine ambayo hayajakusudiwa.

Akikabidhi pikipiki hizo jana kwa maafisa hao Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Adrean Jungu amesema Wizara ya Kilimo imetoa pikipiki hizo ili kuwawezesha maafisa kilimo kufika katika maeneo ambayo hapo awali walikuwa hayafikiki na kuwasaidia wakulima kulima kilimo Bora na chenye tija.

“Leo tunagawa pikipiki nane kwa maafisa kilimo nane wa Halmashauri ya mji ili kuwezesha maafisa hao kufika maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki…vyombo hivi ni vya thamani na vyenye gharama kubwa hivyo ni wajibu wa kila afisa kuvitunza na msije kuonekana mnazitumia kwa matumizi mengine tofauti na yaliyokusudiwa,” amesema Jungu.

Nae, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, David Masanja amesema wizara ya kilimo imefanya jambo kubwa na muhimu sana katika kuhakikisha wanaboresha na kuleta tija kwenye kilimo.

Masanja alisema anaamini kuwa pikipiki hizo endapo zitatumika kwa mlengo uliokusudiwa zitaongeza tija na kasi ya uzalishaji wa mazao .

“Watendaji wakuu tujitajidi sana kutunza vyombo hivi…tutumie kwa mlengo uliokusudiwa ili kuongeza tija katika uzalishaji… mwaka jana kwenye pamba tulivuna tani 5,000 na kwa sasa tumepata vitendea kazi hivyo uzalishaji uongezeke zaidi ya hapo,” Masanja.

Ofisa Kilimo wilaya ya Bariadi, Issa Mtweve amesema wanaishukuru serikali kupitia wizara ya kilimo kwa kuona na kutambua umuhimu wa kukifanya kilimo kiwe na tija kwa kutoa vitendea kazi hivyo.

Mtweve alisema kupitia pikipiki hizo walizopokea ni matarajio yao ni kuwafikia wakulima 17,000 ambao hapo ndani ya Halmashauri hiyo ambapo awali ilikuwa ni ngumu kuwafikia wote .

Nae, Samweli Paul ofisa kilimo kata ya mhango alisema kwa pikipiki hizo zitawasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wao na kuhakikisha wanawafikia wakulima wote na kuwapatia elimu husika juu ya kilimo bora na chenye tija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles