Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amemfukuza kazi Waziri wake wa Ulinzi Gavin Williamson.
Waziri huyo wa Ulinzi amefukuzwa kazi kwa sababu ya kutoa siri juu ya mkutano wa baraza la usalama wa taifa ambapo mawaziri waliijadili kampuni ya China ya mawasiliano ya Huawei.
Kufukuzwa kwa Williamson, ambaye amekanusha vikali kuhusika na uvujishaji wa taarifa hizo, ni pigo jingine kwa May, ambaye nafasi iko mashakani baada ya kushindwa kufanikisha mchakato wa Brexit.
Penny Mordaunt ameteuliwa kuwa waziri mpya wa ulinzi na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza nchini Uingereza kushika wadhifa huo. Hapo awali alikuwa waziri wa misaada ya maendeleo inayotolewa kwa nchi za nje.