WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, amewashukuru madaktari waliopambana kupigania maisha yake, baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona wiki chache zilizolipita.
Boris alinusurika kifo baada ya kuondolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi, lakini sasa hali yake inaendelea vizuri.
Imeelezwa Waziri huyo aliwaandikia ujumbe wa ushukurani, madaktari wote ambao walimhudumia muda wote, ambao alilazwa katika hospitali ya St Thomas.
“Sijui niseme nini, maisha yangu yalikuwa mikononi mwa madokta hawa, hata shukrani zangu hazitoshi kwa jinsi navyojisikia kwasasa, asanteni sana,” alisema Boris.
Msaidizi Mkuu wa Waziri huyo Priti Patel, alithibitisha hali ya kigogo huyo, ambaye aliwapa hofu raia wa Uingereza baada ya kuzidiwa.
“Waziri wetu anaendelea vizuri kwasasa, tunamtakia afya njema na kupona kabisa, anachotakiwa ni kupumzika ili kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Patel.